SHEREHE YA MUUNGANO

Sherehe za kuadhimisha miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA UNAPENDA KUWATANGAZIA KUWA TUMEPOKEA MUALIKO WA SHEREHE YA MUUNGANO ITAKAYOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 30/04/2011. SHEREHE HIYO AMBAYO IMEANDALIWA NA JUMUIYA YA WATANZANIA ROME ITAFANYIKA KUANZIA SAA TISA NA NUSU KATIKA JENGO LA UBALOZI WA TANZANIA ROMA.KWA  WALE  WOTE WATAKAO PATA NAFASI YA KUHUDHURIA WAWASILIANE NA UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA MAKAO MAKUU NAPOLI,ILI TUWEZE KUWAPA TAARIFA WAANDAZI  WA SHEREHE IDADI YA WAGENI WATAKAO FIKA. SHEREHE ZA MUUNGANO NI KUMBUKUMBU MUHIMU YA HISTORIA YA NCHI YETU,HIVYO TUJITOKEZE KWA WINGI KATIKA KUADHIMISHA KUMBUKUMBU HII MUHIMU.
Sherehe za kuadhimisha miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinatarajiwa kufanyika rasmi  Zanzibar tarehe 26 April, 2011 katika Kiwanja cha Aman Mjini Unguja.Taarifa hiyo rasmi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Zanzibar, ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi katika kikao cha Halmashauri hio kilichofanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi wa Mnazi Mmoja. MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!

Kwa mawasiliano piga simu n. 081 0137066  cell. 349 2393714 katibu mkuu.

Post a Comment

0 Comments