Kabla ya mwili kupandishwa ndani ya usafiri,(from L) Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Rome Erasmus Pindu Luhoyo, (c) Kaimu mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italia mama FATUMA TANDIKA na katibu mkuu wa jumuiya ya Watanzania Italia ndugu Kagutta N.Maulidi wakitoa heshima za mwisho. Mwili umeondoka leo na ndege ya shirika la kituruki TURKISH AIR kuelekea Istanbul- Dar. itafika Dar es salaam Tanzania saa 03:35 usiku. Katika shughuli za maombi na kuaga mwili ubalozi wa tanzania Rome uliwakilishwa na Mh Mbilinyi ambae ni mkuu wa utawala ubalozi wa Tanzania Rome. Mh Mbilinyi aliwasilisha salaam za balozi wa Tanzania Rome ambae kwa sababu za kikazi hakuweza kufika na badala yake akatuma ujumbe.
katika salaam za balozi alielezea jinsi gani anaungana na Watanzania wote Italy,ndugu wa marehemu na Wazazi katika kuombopleza msiba huu.Mh Mbilinyi alisema msiba wa mtanzania ni msiba wa ubalozi.katika salaam zake aliwasisitiza zaidi Watanzania kuendelea na ushirikiano,umoja na upendo zaidi. Katibu mkuu wa jumuiya ya Watanzania Italia alikuwa na mazungumzo mafupi na viongozi wa jumuiya ya Watanzania Rome,na wamekubaliana kuitisha kikao cha viongozi wa jumuiya zote za Watanzania nchini Italia ili kuweza kuongelea kwa mapana zaidi kuhusu matatizo ya Watanzania na kutafuta ufumbuzi wa kudumu. Pamoja na hayo kuna mambo zaidi ya muhimu ya kujadili na pengine kuyafikisha ngazi za juu. Kikao hicho kitakuwa mapema mwezi ujao.Kama mwenyeji Mwenyekiti Erasmus Pindu Luhoyo aliitumia nafasi ya kuutambulisha uongozi mpya wa Roma na kuongea kwa kirefu na Watanzania katika kuhimizana na kukumbushana mambo muhimu yanayozunguka jamii ya Watanzania ughaibuni. |
0 Comments