MSIBA ITALY

Marehemu Athuman Omari Wasswar

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania leo tarehe 24/11/2019 uliongoza Watanzania kutoka Napoli ,Rome na sehemu zingine waliohudhuria,kuuaga mwili wa marehemu Athumani Omari Wasswar aliefariki siku ya jumatatu ya tarehe 11/11/2019 akiwa nyumbani kwake. 

Mwili wa marehemu unasafirishwa  nyumbani Tanzania kwa mazishi na utawasili Tanzania siku ya tarehe 28/11/2019. 

Uongozi wa Jumuiya unatoa shukrani kwa wote waliojitolea ndani na nje ya Italy,kwa hali na mali katika kufanikisha taratibu zote za msiba.

katika hotuba ya kuaga mwili wa marehemu,pamoja na kutajwa wasifu wa marehemu ,mwenyekiti wa Jumuiya ya 

 Watanzania Italia ndugu AbdulrahamanA.Alli,aliwashukuru sana watanzania wote kwa ushirikiano mkubwa waliotoa kwa kufanikisha zoezi zima kwa kipindi kifupi. 

Mwenyekiti alisisitiza mshikamano zaidi kati ya Watanzania na jumuiya zake. Mwisho kabla ya dua ya pamoja katibu wa jumuiya wa Napoli alitangaza kuwepo kwa mkutano wa Watanzania siku ya tarehe 26/11/2019 katika ofisi  za Jumuiya muda wa  jioni saa kumi na moja,kujadili mustakabali mzima wa jumuiya pamoja na uchaguzi wa kamati ya fedha.
 innalillah wainna illah raj uun.

 Chini ni baadhi ya picha za tukio zima la kuaga mwili wa marehemu. 

Kassa Musa mchezaji wa zamani wa Coastal Union ya Tanga alikuwa mmoja wa Watanzania walioshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Athumani Omari Wasswar .



















Post a Comment

1 Comments

GFAMILY said…
poleni sana ndugu zetu