TANZANIA


RE: HAKI ZA WATOTO WA KIKE[BWIRU SEKONDARI]

udaku
Ndugu Watanzania,
Napenda nielezee mambo niliyoyaona kwa macho yangu katika shule hii kongwe ya Bwiru iliyopo manispaa ya Mwanza. Ni jambo la kushangaza na kutia aibu sana kuwa shule hii kongwe ya wasichana haina vyoo na mabafu ya kuogea.

Nimetembelea Mkoani mwanza nikitokea kushuhudia uchaguzi ya Tarime ambao kwa kiasi fulani ulitufundisha Mengi sana hususani utawala wa nchi kwa ujumla. Katika harakati za kutaka kumtembelea Mwanangu anayesoma katika Shule hii ya Bwiru Mkoani Mwanza nilikutana na kizaa zaa cha watoto kunieleza kuwa shule yao kwanza haina vyoo vya kutosha na pia hawana maji safi na salama na la Mwisho lililotia aibu kabisa ni mahali pa kuoga wao na ukichukulia ni wanafunzi wa kike. Kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana na wanafunzi wengine walidiriki kutoa machozi wakati wakieleza jambo hili kwa mkazo kabisa kuwa pia kwenda kuoga ziwani kunawahatarishia wao kubakwa na wavuta bangi wanaokuwepo Ziwani mara kwa mara.
Tulipata Uhuru mwaka 1961 lakini nafikiri Uhuru wetu sio kamili iwapo tutakuwa tunawanyanyasa watoto wetu kiasi hiki.Nawatuma Waandishi wa habari popote mlipo mjini Mwanza na Dar es salaam ikiwa ni pamoja na Wanawake mnaosimamia haki za wanawake Duniani muende kuhakikisha haya niyasemayo na mumfikishie Waziri anayehusika na pia ikishindikana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama kuna waandishi wa kike naomba mkereke na tabia hii ambayo mimi nadhani inasababishwa na uongozi wa shule ya Bwiru. Sidhani kuwa wanafunzi wangehamasishwa wangeshindwa kujichangia wao wenyewe wajenge hata banda la mabati kwa ajili ya kuogea kukwepa adha ya kuogea Ziwani na pengine kuingia kwenye hatari ya wao kubakwa.

Inatia huruma sana kuona watoto wa kike kama hawa wanaoga ziwani na p engine kushikwa na maradhi ya kichocho na hata malaria kwa ajili ya huduma mbaya za upatikanaji wa maji. Hivi Tanzania tunataka kujenga taifa la namna gain?. Kwa wale wanawake ambao mtapata barua hii pepe nawasihi sana tembeleeni shule hii mujionee malezi wanayopewa watoto wa kike katika Shule hii. Kweli kuoga hadharani kwa watoto kike na hata wa kiume ni malezi bora kwa mototo wa Kitanzania?.
Mkereketwa
Ole Sailepi.


IMETOLEWA NA: http://www.globalpublisherstz.com

Post a Comment

0 Comments