Marehemu Moses Kiumbi aagwa Rome





Pichani mwili wa marehemu ukisaliwa.
Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Tawi la Roma unapenda kutoa shukurani za dhati kwa wale wote waliofika kumuaga Marehemu Moses Kiumbi jana tarehe 31 oktoba mjini Roma, kabla ya kusafirishwa kwenda Tanzania. Moses alifariki tarehe 22 Oktoba 2009 kwenye Hospitali ya Umberto I Roma ,ambapo alikuwa anapatiwa matibabu baada ya kuanguka baada ya kushuka kwenye Bus tarehe 17 Oktoba 2009. Uongozi unapenda kuwashukuru Watanzania wote waliokuja kwa wingi wakitokea Napoli, Modena na Genova. Viongozi pia unatoa shukurani za dhati kwa Ubalozi wetu wa Tanzania hapa Italy kwa kutusaidia kwa Documentations na misaada mingine mbali mbali.
Marehemu Kesho 2 November ndio atasafirishwa na ndege ya KLM itakayoondoka Rome Fiumicino Airport saa mbili na dakika kumi za usiku na kufanya Transit Amsterdam kwenye mida ya saa tano asubuhi siku ya jumanne tarehe 3 Oktoba. Marehemu anategemewa kuwasiri Mwalimu Jurius Kambarage Nyerere Airport Dar-Es-Salaam, siku ya Tarehe 3 November saa tano na dakika thelathini na tano za usiku ambapo atapokelewa na ndugu zake. Mungu amlaze mahali pema ndugu Moses Kiumbi. Kwa habari zaidi na Picha zaidi tembelea blog ya Jumuiya ya Watanzania Tawi Roma hapa: http://www.watanzania-roma.blogspot.com/

Andrew Chole Mhella
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Tawi la Roma

Post a Comment

0 Comments