DIASPORA NEWS: NALA MONEY KUSHIRIKIANA NA EQUITY BANK

 

Benki kuu ya Tanzania (BOT) imeipa idhini Kampuni ya Teknolojia ya huduma za kifedha ya NALA MONEY  kuweza kutoa huduma zake hapa Tanzania kwa ushirikiano na Equity Bank Tanzania.

Tanzania ilikuwa ni Nchi ya kwanza NALA kuomba idhini lakini ilipata kibali na kuanza kutoa huduma zake kwenye nchi za Kenya, Uganda na Uingereza kabla ya Tanzania, habari njema ni kwamba tayari BOT imeiruhusu NALA kutoa huduma zake kwa watumao fedha kutoka Uingereza kuja Tanzania kwa kupitia ushirikiano na Benki ya Equity.

"Naishukuru Benki Kuu ya Tanzania kwa kutuamini na ninafurahi sana kuona teknolojia ya nyumbani inavuka mipaka na kufikia watu wengine duniani, naamini Mungu ametupa uwezo wa kufanikisha hilo” ——— Benjamin Fernandes Mwanzilishi wa NALA.

Hivi karibuni AyoTV itafanya Exclusive Interview na Fernandes kufahamu zaidi. #MillardAyoUPDATES

Post a Comment

0 Comments