TAWI LA CCM ITALY

pichani kutoka kushoto ni katibu wa tawi ndugu Kagutta N.Maulidi, Mwenyekiti wa tawi,ndugu Abdulrahaman A.Alli, katibu siasa (mwenezi) ndugu Allan Bendera na mwisho ni katibu uchumi mama Fatuma A.Tandika.
Pichani, Viongozi na wajumbe wa tawi jipya la chama cha mapinduzi  Napoli Italy katika picha ya pamoja.Tawi la CCM Napoli ni tawi la kwanza la chama cha mapinduzi  nchini Italy.

Tarehe 25/03/2010 ni siku  inayoingia katika historia ya Chama cha Mapinduzi nchini Italy,baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa kwanza wa kuchagua viongozi wa tawi la CCM Napoli.Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wakereketwa wanachama hai wa CCM ughaibuni ,ulimalizika kwa furaha na mafanikio makubwa. Katika uchaguzi wa viongozi wa tawi hilo, ndugu ABDULRAHAMAN A.ALLI alichaguliwa kuwa Mwenyekiti,Wana CCM pia walimchagua ndugu KAGUTTA N.MAULIDI  kushika nafasi ya katibu wa tawi. Nafasi ya katibu siasa ilichukuwa na ndugu ALLAN BENDERA na mama FATUMA A.TANDIKA alichaguliwa kuwa katibu uchumi. Pia katika uchaguzi huo Bi JUDITH JOSEPH, Bi ZENA HASSAN ,ndugu AWADH SALIM na Mzee HAMISI MNYAMANI  walichagualiwa kuwa  Wajumbe wa CCM tawi la Napoli.

   Abdulrahaman A.Alli(mw/kiti)                  Kagutta N.Maulidi (katibu)
     Allan Bendera (katibu siasa)            Fatuma A.Tandika (katibu uchumi)
       Awadh S.Saleh (mjumbe)                  Judith Joseph (mjumbe)
      Hamisi Mnyamani (mjumbe)                    Zena Hassan (mjumbe)

Post a Comment

2 Comments

Anonymous said…
Inaonekana CCM haiepukiki. Hata tuliokimbia Tanzania naona inatufuata huku huku tuliko. Naona hata Jehanamu itakuwako. Duh!!!

Msibanie comment yangu please
Anonymous said…
This comment has been removed by a blog administrator.