Siku ya jumapili jioni Watanzania waishio Napoli na vitongoji vyake kwa pamoja walikusanyika katika kusherehekea sikukuu ya pasaka. Sherehe hiyo iliyoandaliwa na akina dada wa kitanzania wanaoishi Napoli iliendelezwa kwa muziki ,vinywaji na nyama choma. Blog hii inatoa pongezi nyingi kwa kina dada wote kwa kutufanya tujisikie tuko nyumbani tukiwa ughaibuni pongezi kwa maandalizi mazuri na kwa mapichi mazuri ya mahanjumati. Kitendo hiki ni moja ya malengo ya jumuiya ya Watanzania Italy kuwaunganisha Watanzania na kujenga umoja na ushirikiano.
PICHANI NI POZI ZA PASAKA
Kwa picha zaidi za pasaka GONGA HAPA
(picha zote kwa hisani ya katibu wa habari George Mayaka)
1 Comments
Panyabuku,