SALAAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA MSIBA WA HAYATI MAALIM SEIF MAKAMU WA KWANZA WA RAISI ZANZIBAR

Hayati Maalim Seif

 

Jumuiya ya Watanzania nchini Italy, imepokea taarifa za msiba wa kiongozi wetu Maalim Seif aliyekuwa makamu wa kwanza wa Raisi wa Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu na kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa. Jumuiya ya Watanzania Italy (Diaspora) tunaungana na Watanzania wote na wananchi wenzetu wa Zanzibar katika kuomboleza msiba huu mkubwa kwa taifa. Tunatoa pole kwa Raisi wa Zanzibar Mh Dr Hussein Mwinyi, familia ya marehemu, Chama chake cha siasa ACT na kwa Watanzania wote. Ni imani yetu tutaendelea kumuenzi kwa kuendeleza  utulivu ,amani na maridhiano aliyopigania katika uhai wake. Tunamuomba MwenyeziMungu ailaze roho yake mahala pema.

( INNALILLAH WAINNA ILLAH RAJ UUN)

Kwa niaba ya Jumuiya,

Abdulrahman A.Alli

Mwenyekiti


 

Post a Comment

0 Comments