SALAAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA KUFUATIA MSIBA WA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI


 Jumuiya ya Watanzania Italia, tumepokea taarifa za msiba wa Amiri jeshi mkuu,Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Daktari John Pombe Joseph Magufuli ,taarifa ziliotangaza rasmi na Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan. Taifa letu limepata msiba mkubwa, Msiba wa Taifa, Kwa niaba ya Watanzania wote tuishio Italia (DIASPORA) tunapenda kuungana na Watanzania wote walio ndani ya mipaka na nje ya mipaka ya nchi yetu,katika kuomboleza msiba huu mkubwa kwa taifa letu. 

Tunatuma salaam zetu za rambirambi kwa Makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri mkuu Mh Majaliwa Kasim Majaliwa, Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Hussein Ali Hassan Mwinyi, serikali zote, Chama cha Mapinduzi na Wanachama wote na zaidi kwa Watanzania wote.

Mwisho kwa umuhimu wa pekee tunatuma salaam hizi za Rambirambi na pole kwa MAMA JANET MAGUFULI, WATOTO NA FAMILIA NZIMA  YA DR JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.

Katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na mtihani mzito kwa Taifa letu Tunamuomba MwenyeziMungu atupitishe salama na kutupa faraja kama Taifa.

Mola ailaze Roho ya mpendwa wetu, shujaa wetu mtetezi wa wanyonge,mpambanaji, mwana mageuzi na maono mahala pema peponi.


R.I.POWER JPM


 

Post a Comment

0 Comments