EQUITY BANK (T) LTD YAZINDUA KAMPENI MPYA YA KUWEKA AKIBA (JIJENGE)

 

Equity Bank (T) leo imenzidua rasmi akaunti maalum ya utunzaji fedha kwa kujiwekea kidogo kidogo ili kufikia malengo ijulikanayo kama “Jijenge Akaunti”.
Akaunti ya Jijenge ni mpango wa kujiwekea akiba (savings plan) wenye lengo la kuboresha maisha ya watanzania kwa kuwapa fursa yakujiwekea akibaKadri wanavyopata ili kufanikisha mipango yao ya maisha ikiwemo kujenga nyumba, kununua viwanja, kulipa karo na mengineyo.
Akizungumza katika hafla ya uzunduzi wa akaunti hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Equity (T) Isabella Maganga amesema kuwa Jijenge akaunti ni suluhisho rasmi la kujiwekea akiba na kufikia malengo.
 “Kupitia akaunti hii ya Jijenge mteja anapata nafasi ya kufikia mipango yake ya muda mrefu au mfupi kwa kujiwekea akiba taratibu na hatimaye kufikia malengo. Jijenge akaunti ni daraja la kufikia ndoto za Maisha kupitia kujiwekea akiba. Kubwa Zaidi ni kuwa ukiweka akiba kwa kipindi cha miezi sita na kuendelea, unaweza kukopa mpaka mara tatu ya fedha ulizojiwekea” alisema.
 Akizungumza kuhusu taratibu za ufunguaji na uendeshaji wa akaunti hiyo ya Jijenge; Bi.Masanja alisema “Ili kufungua akaunti ya Jijenge, mteja anahitaji kuwa na kitambulisho cha NIDA pekee,  na kianzio ni shilingi elfu kumi tu. Kama ilivyo kwa akunti zetu zingine, Jijenge akaunti pia haina makato yoyote ya mwezi na inajipatia riba nzuri na endelevu.
Pia tumeweka urahisi wa kujiwekea akiba kwa kuwapa wateja wetu uwezo kutuma pesa kwenye akaunti zao za “Jijenge” kwa kutumia huduma yetu ya Simu za mikononi “Eazzy Banking” huduma kupitia mtandao wa intanenti yaani “Eazzynet” au kwa kutumia utaratibu maalum kuhamisha fedha yaani Standing Order”alisema.
Maelezo zaidi kuhusu Jijenge Akaunti
• Uwezo wa kupata mkopo mara Tatu ya kiwango cha akiba ulichojiwekea ndani ya miezi sita na kuendelea.• Kiwango cha chini cha kufungua cha shilingi elfu kumi • Haina makato ya kila mwezi• Kitambulisho cha NIDA kinatosha  kufungua  akaunti • Riba endelevu• Njia rahisi za kuweka pesa • Ruhusa kufungua kwa Vikundi • Bima kwa mikopo yote
Kuhusu Equity BankEquity Bank Tanzania Limited ni taasisi ya kifedha inayofanya kazi nchini Tanzania chini Equity Group Holdings Plc iliyo na matawi katika nchi nyingine za Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini, Rwanda, Congo (DRC).Kwa sasa Equity ina matawi 15 na Mawakala zaidi 3,600 nchi nzima, ATM na huduma za kibenki kupitia Simu za mkononi na Intaneti.














 

Post a Comment

0 Comments