JIJENGE ACCOUNT NA DIASPORA FURSA YA KUJIJENGA

JIJENGE ACCOUNT  NA DIASPORA
Equity Bank (T)  imenzidua rasmi akaunti maalum ya utunzaji fedha kwa kujiwekea kidogo kidogo ili kufikia malengo ijulikanayo kama  “Jijenge Akaunti”
Akaunti ya Jijenge ni mpango wa kujiwekea akiba (savings plan) wenye lengo la kuboresha maisha ya watanzania pamoja na  DIASPORA kwa kuwapa fursa yakujiwekea akiba Kadri wanavyopata ili kufanikisha mipango yao ya maisha ikiwemo kujenga nyumba, kununua viwanja,mengineyo.
Jijenge akaunti ni suluhisho rasmi la kujiwekea akiba na kufikia malengo.


 “Kupitia akaunti hii ya Jijenge mteja anapata nafasi ya kufikia mipango yake ya muda mrefu au mfupi kwa kujiwekea akiba taratibu na hatimaye kufikia malengo. Jijenge akaunti ni daraja la kufikia ndoto za Maisha kupitia kujiwekea akiba. Kubwa Zaidi ni kuwa ukiweka akiba kwa kipindi cha miezi sita na kuendelea, unaweza kukopa mpaka mara tatu ya fedha ulizojiwekea”


Kianzio ni shilingi elfu kumi kwa TU Kama ilivyo kwa akunti zetu zingine, Jijenge akaunti pia haina makato yoyote ya mwezi na inajipatia riba nzuri na endelevu.
Tuma pesa kwenye account yako ya Jijenge kwa kutumia huduma yetu ya “Eazzy Banking” huduma kupitia mtandao wa intenet yaani  “Eazzynet”  au kwa kutumia utaratibu maalum kuhamisha fedha yaani Standing Order”, WESTERN UNION, MONEYGRAM, WORLDREMIT


Fursa za kufungua  akiba ya Jijenge
•    Uwezo wa kupata mkopo mara Tatu ya kiwango cha akiba ulichojiwekea ndani ya miezi sita na kuendelea.
•    Kiwango cha chini cha kufungua cha shilingi elfu kumi tu
•    Haina makato ya kila mwezi
•    Riba endelevu ya 3%
•    Njia rahisi za kuweka pesa
•    Ruhusa kufungua kwa Vikundi
•    Bima kwa mikopo yote


Kuhusu Equity Bank
Equity Bank Tanzania Limited ni taasisi ya kifedha inayofanya kazi nchini Tanzania chini Equity Group Holdings Plc iliyo na matawi katika nchi nyingine za Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini, Rwanda, Congo (DRC).
Kwa sasa Equity ina matawi 15 na Mawakala zaidi 3,600 nchi nzima, ATM na huduma za kibenki kupitia Simu za mkononi na Intaneti.


#LIVEGLOBALLYBANKLOCALLY 


 

Post a Comment

0 Comments