SOUTH AFRICA: MTANZANIA AKAMATWA SA KWA KUCHOMA MOTO

 

Na Aboubakary Liongo

Moonlight MediaPhoto by SABC

Mtanzania Frederick Mhangazo (38)anefikishwa kwenye mahakama ya Cape Town Afrika Kusini akikabiliwa na makosa ya kusababisha moto uliyoteketeza takriban heka 600 jijini humo.Moto huo uliyowaka Jumapili iliyopita umeteketeza nyumba na taasisi kadhaa jijini Cape Town ikiwemo sehemu ya chuo kikuu.Msemaji wa mamlaka ya taifa ya mashtaka katika jimbo la Westen Cape Eric Ntabazalila amesema mtanzania huyo alikamatwa upande wa pili wa mlima(Table Mountain) Jumapili jioni na hakufanya jaribio lolote la kutaka kukimbia.Wakili wa mtanzania huyo Shaun Balram ameiambia mahakama kwamba mteja wake anashutumiwa kimakosa na kuongeza hana historia yoyote ya uhalifu inayoweza kuleta hisia kuwa anahusika. Ameimbia zaidi mahakama kuwa kijana huyo anaishi katika mabanda yasiyo ya kudumu kwa hivyo ili kujua kuwa ni kweli anaishi kwenye eneo lamabanda alipokamatwa ni lazima kuwauliza wakazi wa maeneo ambayo amekuwa akionekana sana.Moonlight Media imezungumza na watanzania wanaoishi jijini Cape Town ambao wamesema Mhangazo ni miongoni mwa watu wanaolala mabarabarani.“Mshikaji ni wale watu wanaolala kwenye machaka.. sasa moto ulivyotokea wajomba(polisi) wakavamia eneo lile wakawakurupusha jamaa akadakwa.Lakini mshikaji hana nguvu wala akili ya kuchoma moto…hana kabisa uwezo huo” alisema mtanzania huyo ambaye alikataa kunukuliwa jina lake.Kesi imeahirishwa hadi tarehe 28 mwezi huu ili kupata uhalali wa mtuhumiwa kupewa dhamana.


 

Post a Comment

0 Comments