Mama Fatuma Abedi Tandika anayofuraha kuwaalika Watanzania wote wanaoishi Napoli na nje ya mkoa katika kisomo na dua kwa ajili ya kumbukumbu ya marehemu mume wake prof.Abedi Tandika aliyefariki mwaka 2006 mwezi wa Ramadhani. Kisomo na dua kwa marehemu zitambatana na Futari siku ya tarehe 4/9/2010 nyumbani kwa mama Tandika- CASTEL VOLTURNO CE. wote ambao wako katika mfungo wa Ramadhani wafike bila hofu kwani futari itakuwa tayari kwa wote. BLOG HII INAPENDA KUUNGANA NA FAMILIA YOTE YA PROF. TANDIKA KATIKA KUMBUKUMBU YA MZEE WETU. RIP.
1 Comments
Profesa Tandika tulikuwa wote Chuo Kikuu Dar es Salaam, kama walimu na watafiti. Alikuwa mwema na mcheshi. Kukutana naye ilikuwa ni baraka, kwani alikuwa na kipaji cha kukufanya ufurahi.
Bahati mbaya, labda kwa vile nakaa mbali, sikuwa na taarifa kuwa alituaga duniani. Nasikitika. Lakini, kwa jinsi alivyoishi nasi kwa ubinadamu, nafarijika kuwa Mungu atamrudishia maradufu huko aliko. Astarehe kwa amani. Amina.