Watanzania wakiwa katika sura za majonzi wakati wa kikao cha kukamilisha taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu CLEAN HEART aliyefariki siku ya tarehe 8/12/2013 mjini Rome. Mbele yao ni picha ya marehemu.
Pamoja na kuwa bado kunahitajika michango zaidi kukamilisha taratibu za safari ya mwisho ya marehemu, lakini hata hivyo upo uwezekano wa kuwepo kwa safari ya kwenda Rome sikuu ya jumamosi kuuaga mwili wa marehemu Abdulli Abuu kwa wakazi wa Napoli na vitongoji vyake" katibu wa jumuiya ya watanzania Italia Napolii ndugu Livinus Mwereke aliwatangazi watanzania waliohudhuria katika kikao cha leo jioni kilichofanyika Penitamare Caserta. Kaimu Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia aliwashukuru wote kwa kujitolea kwa hali na mali katika kufanikisha zoezi hili gumu, Mama Fatuma Tandika pia aliwashukuru viongozi wote wa jumuiya za watanzania nchini Italia kwa kuwa mstari wa mbele na kujitolea bila kuchoka katika matukio makubwa yanapotokea. Pia alisistiza kuendeleza upendo na umoja baina ya Watanzania wote.
|
0 Comments