MKUTANO WA WATANZANIA NAPOLI







Viongozi wa jumuiya  baada ya mkutano



Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania (presidente della comunità Tanzaniana in Italia) Mh.Abdulrahaman A.Alli akiwa na katibu mkuu ndugu Kagutta NM.  na katibu wa jumuiya Napoli mjini ndugu Mwereke Livinus  katika mkutano wa Watanzania wanaoishi Napoli. Mkutano huo uliofanyika tarehe 22/01/2009 katika ukumbi wa CGIL ,ulimalizika kwa mafanikio makubwa.Viongozi walitoa ripoti ya maendeleo ya jumuiya katika kipindi chote cha mwaka 2009 na kufafanua juu ya malengo mapya ya 2010-2011.Mwenyekiti alisisitiza umoja na ushirikiano zaidi baina ya Watanzania na wanyeji (wataliani) ,mwenyekiti pia alionya juu ya machafuko ya kibaguzi, ..alisema  kwa kweli kama tukifuata sheria za nchi tunayoishi sidhani kama kutakuwa na matatizo,pia alisisitiza si kweli kuwa wataliani ni wabaguzi kwani kama wangekuwa wabaguzi tusingekuwepo hapa...cha muhimu ni kufuata sheria za nchi zilizowekwa na kama kuna matatizo hata sehemu za kazi basi tufuate sheria ambazo zipo kumlinda kila mtu. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na baadhi ya wataliani ambao kwa kweli wameonyesha kuvutiwa na jumuiya ya watanzania Italy na kupenda kujua zaidi kuhusu nchi yetu ,lugha na utamaduni wetu.

Post a Comment

0 Comments