SALAAM ZA CHRISTMASS NA MWAKA MPYA



Salaam za Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia

Tumejaaliwa kupata fursa ya kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Kristo huku tukisubiria sikukuu ya  Mwaka Mpya.
Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania Italia na viongozi wote wa jumuiya na matawi yake, na kwa niaba yangu binafsi napenda kushirikiana nanyi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kufikia kipindi hiki muhimu.
Katika kusherehekea sikukuu hizi muhimu natumaini tutakuwa na fursa nzuri ya kutembeleana na kuimarisha mshikamano kati yetu na kusherehekea kwa amani.
Nawapeni nyote mkono wa heri ya Krismas,  na kuwatakia kheri ya Mwaka Mpya 2011
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
ABDULRAHAMAN A.ALLI
Mwenyekiti (JUWATAI)

Post a Comment

0 Comments