Ndugu Watanzania wenzangu na wote wenye mapenzi na nchi yetu mlioko hapa Italy . Tumejaaliwa kupata fursa ya kusherehekea sikukuu ya Eid El-Fitri kwa salama na amani. Kwa niaba ya Mheshimiwa A.A KARUME Balozi wa Tanzania hapa Italy, na kwa niaba ya Viongozi wenzangu wa matawi yote ya jumuiya hapa Italy na kwa niaba yangu binafsi napenda kushirikiana nanyi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kufikia kipindi hiki muhimu. Tangu kuanzishwa kwa jumuiya yetu, tumekuwa tukijitahidi kuwajibika na kushirikiana kwa namna mbalimbali na Watanzania walioko hapa. Katika kipindi hiki pia tumejitahidi kupigania kuimarisha mshikamano wa Watanzania na hatimaye kufanikiwa,ingawa bado kuna wachache wenyi nia tofauti. Ni matumaini yetu kuwa Watanzania watailinda na kuiinua Jumuiya yao kwa mafanikio yao na Taifa letu kwa ujumla. Watanzania tuna sifa kubwa ya kuheshimiana, kuvumiliana na kushikamana bila kujali itikadi zetu za kisiasa, imani zetu za dini au kabila au rangi. Ni matumaini yetu tutaendelea kudumisha mshikamano wetu siku zote tukifanya kazi kwa bidii ili tuchume ugenini na kuweza kuijenga nchi yetu na kuwa mabalozi wazuri wa nchi yetu,pia kushirkiana na wenyeji wa nchi tunamoishi na kufuata sheria za nchi hii (Italy)kama ilivyo. Katika kusherehekea sikukuu hii muhimu natumaini tutakuwa na fursa nzuri ya kutembeleana na kuimarisha mshikamano kati yetu. Nawapeni nyote mkono wa Eid El Fitri, na kuwatakia kila la kheri. AUGURI TUTTI!!
Abdulrahaman A.Alli
Presidente della comunità Tanzaniana in Italia.
1 Comments
Mdau mpenda nchi