NAPOLI: MSIBA

JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTANZANIA MAREHEMU  MAULIDI  HAMID ABDALLA  MAARUFU KWA JINA LA KIDISHI.

Kidishi amefariki  siku ya jumanne ya tarehe 7/01/2014  usiku . Marehemu amefariki katika hospitali ya  COTUGNO mjini Napoli, baada ya kulazwa kwa muda wa wiki tatu.

Marehemu katika uhai wake amewahi kucheza mpitra timu ya Black Fighters  na hata Timu ya taifa zote za Zanzibar  katika miaka ya themanini.

Mipango ya mazishi inafanywa na tayari yameshafanyika mawasiliano na familia ya marehemu.

TUNAPENDA KUWATANGAZI WATANZANIA WOTE KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA HARAMBEE YA KUCHANGIA MIPANGO YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI KWA MAZISHI , MKUTANO UTAFANYIKA PALEPALE ULIPOFANYIKA MKUTANO WA KWANZA WA MAREHEMU JUMA KIJUU.

MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA.. AMIN!

Post a Comment

0 Comments