BIRHDAY PARTY !

Mwenyekiti wa jumuiya ya watanzania italy Mh.ABDULRAHAMANI A. ALI akiwa na mama TANDIKA katika picha ya pamoja na Mapozi na Mary.Wao walishuhudia tukio hili kwa niaba ya wazazi wa pande zote mbili. Baada ya hapo Mwenyekiti alipewa wasaa wa kuzungumza machache na kutoa nasaha zake kama mzazi,mwenyekiti pia alisisitiza tendo kama hili tunategemea litakuwepo kwa wengine kwani huu ni mfano mzuri na ndio hasa maadili tuliyolelewa nayo sote huko makwetu,tuache mambo ya kujifificha ficha kwani yana madhara makubwa hasa katika wakati huu ambao sote tunaelewa''alisisitiza mwenyekiti'' Mwisho aliwashukuru wale wote waliojitolea muda wao katika kumfanikishia shughuli mwenzetu na pongezi nyingi kwa dada JUDDY ambae aliongoza shughuli yote kwa ujumla na kutoa burudani ambalo sote tuliburudika baada ya kuimba nyimbo ya WHITNEY HUSTON !
Tukio zima lilikamilishwa hivi! hii ni kutoa taarifa rasmi kuwa jamani hapa mimi ndo nimezimika!
wakilishana keki katika mchongo mwingine!

Ilikuwa ni birthday party ya kijana Salim .AKA. Mapozi ndipo ghafla kijana aliamua kuhitimisha siku yake ya kutimiza 25yrs kuwa ndo siku ya kumchumbia binti mmoja mrembo kuwa ndie chaguo lake na ndie atakae kuwa mywife wake muda si mrefu.

Post a Comment

0 Comments