SHEREHE ZA MIAKA 51 YA MUUNGANO ZAFANA JIJINI ROMA, ITALIA



ROME: Ubalozi wa Tanzania Roma, kwa kushirikiana na Tanzania Diaspora ya Italia
tarehe 25 Aprili 2015 walisherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sherehe hizo ambazo zilifanyika katika ukumbi wa Ubalozi mjini Roma zilifana sana.

Mhe. Balozi Dr. James Alex Msekela ( mwenye tie) akigonganisha bilauri na Bw. S. M. Mbilinyi, Mkuu wa Utawala, katika sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya Muungano wa Tanzania. Sherehe hizo zilifanyika Ubalozini Roma jioni ya terehe 25 Aprili 2015.
Baadhi ya Watanzania walioshiriki kwenye sherehe za muungano wakiimba wimbo wa kuisifu Tanzania( Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote)
Mhe. Balozi (kati) akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyekiti wa Diaspora (kulia) na baadhi ya Watanzania wanaoishi  Napoli.
Afisa wa Ubalozi, Bw. Amon Ruvurula (kulia) na Bw. Seraphino Makole wakifurahia sherehe za Muungano.
Afisa wa Ubalozi, Bw. Karim Msemo, na mke wake wakiwa kwenye picha  na Bi. Felista Kayombo, ambaye pia ni mtumishi wa Ubalozi.
Mhe. Balozi Msekela akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa Tanzania Diaspora in Italy, Bw Andrew Mhella (kulia) na Bw.Mnyamani kutoka Napoli
Bw. Ayoub Mndeme, Mwambata Kilimo akiwa na mama Mndeme kwenye sherehe za Muungano.
Kutoka kushoto: Bakari, Mbilinyi na  Lilian wakiwa na nyuso za furaha kwenye sherehe za Muungano
Mama Balozi Msekela (aliyesimama katikati na gauni la brown)  akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania  kina mama waishio Italia, waliofika Ubalozini kwa sherehe za Muungano hapo 25 Aprili 2015.








Post a Comment

0 Comments