Hayati Ndalima Yusuph Nzaro
*****************
Kwa masikitiko makubwa Familia ya Mohamed Nzaro na Balozi Eva Nzaro inatangaza kifo cha mtoto wao Ndalima Yusuph Nzaro kilichotokea siku ya Alhamisi Katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan mjini Ann Arbor ambapo alikuwa amekimbizwa kutibiwa baada ya ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia Jumanne ya Oktoba 14, 2008.
Gari alilokuwa akiendesha marehemu liligongwa na gari nyingine wakati likisubiri taa za kuongozea magari.
Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania kwa mazishi inaendelea. Vile vile, utoaji wa heshima za mwisho mjini Detroit unatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 18 Oktoba, 2008. Muda rasmi utatangazwa baada ya maandalizi kukamilika.
Familia inapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru na kuwaomba msaada wenu wa hali na mali katika kufanikisha safari hii ya mwisho ya kijana wao mpendwa Ndalima.
Michango kwa ajili ya msiba huu inaweza kupelekwa moja kwa moja kwenya akaunti maalum ifuatayo:
Bank Of America:
A/C Name: Mboja Nzaro (Dada wa Marehemu)

Routing No. 072000805A/C No. 5407722411

Mawasiliano zaidi Kuhusu habari za msiba huu wasiliana na wafuatao:
Anna Royal Mfinanga 248-778- 6395
Abdul Kufakunoga 248-515- 5509
Salum Ndolanga 248-796-1267
Philemon Mnzava 248-417-5015Leo
The Saint 614-426-3422
Msiba huu kwa Detroit unafanyika nyumbani kwa binamu yake Ayubu Mfinanga.

Anuani ya Kwa Ayub:
22255 HesselDetroit, MI 48219
Tutaendelea kuwahabarisha kwa kadiri mipango inavyoendelea.
Asanteni kwa sala zenu, ushirikiano wenu na misaada yenu.

FAMILIA YA NZARO
MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALY ,KWA NIABA YA VIONGOZI NA WANAJUMUIYA WOTE,TUNAPENDA KUJUMUIKA NANYI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAJONZI MAKUBWA,SISI TUMESIKITISHWA SANA NA MSIBA HUU INGAWA NI KAZI YA MUNGU.TUNATOA SALAM ZETU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU ,NDUGU JAMAA NA MARAFIKI, TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI AMIN!!

Abdulrahman A.Alli
Mwenyekiti.

Post a Comment

0 Comments