MATAWI YA NJE YA CCM YALIALIKWA KATIKA MKUTANO MKUU 2010





Mwenyekiti wa tawi la CCM  Italy (Napoli) ndugu Abdulrahaman A.Alli na Katibu wa Tawi hilo  ndugu Kagutta N.Maulidi walihudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika mjini Dodoma julai 10-11, 2010, Tawi la Chama cha Mapinduzi Napoli ni tawi la kwanza na pekee kufunguliwa Italy kufuatana na katiba ya CCM kuhusu matawi ya Chama cha Mapinduzi ya nje ya nchi.Pichani juu Mwenyekiti wa tawi la Napoli (Italy) ndugu Abdulrahaman A.Alli akiwa na Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa Mh.Membe wakiwa katika mapumziko ya lunch mjini Dodoma (Kizota) picha ya kati ni Mwenyekiti na katibu wakati wa mapumziko .

Post a Comment

2 Comments

Anonymous said…
Aaah! Huu ni upuuzi wenu.. Mlikwenda Tanzania kumsaidia kampeni za Ubunge kwa mswahiba wenu Joel Bendera .... matokeo yake mlivuna pepo baada ya kupanda tufani... Watanzania tunazema hatudanganyiki!!! kidumu Chadema!! Chama ambacho hakikumbatii mafisadi!!!
Hamisi Ayubu, Muheza, Tanga.
Anonymous said…
vibaraka nyie, kwa ujinga wenu.. mkamuuza ndugu yetu Joel Bendera kwenye kampeni za Ubunge... kapigwa teke nje!!! Nyie ndugu zetu, Ulaya kumewashinda...na mnakuja sasa kuwekeza kwenye vyama vya siasa... hovyo... mitanzania bana.. Unafiki tupu... mtu kafika Ulaya lakini bado mnaona ufahari kuweka picha za kuwa pamoja na Kikwete....ili???

Kumbukeni kuwa tunawajua mnafanya nii, huko Ulaya...afadhali mrudi tu hapa nyumbani muungane nasi maskini wa Kikwetu kwenye kilmo kwanza...
Shaban Mhina.. Muheza