Mtoto Tatyanna J ndie aliyekuwa Miss Chuchu katika sherehe za Eid El Fitri zilizofanyika Napoli. Pichani akiwa na zawadi nono baada ya kushinda ingawa watoto wote walipata zawadi.
Mr chuchu Amini aka Ronaldinho akipongezwa na mwenyekiti wa kamati ya sherehe Lady Judy pamoja na Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy.
Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy ,Mh.Abdulrahaman A.Alli alichukua nafasi ya kuwashukuru wote walijitolea kwa hali na mali katika kufanikisha sherehe ya Eid, pia alimpongeza mwenyekiti wa kamati ya sherehe Lady Judy kwa matayarisho mazuri mpaka kufanikisha sherehe hasa kwa upande wa watoto.Mwenyekiti aliwatakia kila kheri katika Eid watanzania wote waishio Italy pamoja na ubalozi wa Tanzania Rome.Mwenyekiti alisisiziza ushirikiano zaidi kati watanzania na wenyeji (Italian).



0 Comments