MWENYEKITI WA JUMUIYA MSTAAFU AKABIDHI NYARAKA RASMI KWA MWENYEKITI MPYA

 

 JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA (IN CAMPANIA) WAFUNGUA UKURASA MPYA

 

Tarehe 13/08/2022 kulifanyika makabidhiano rasmi ya nyaraka muhimu za usajili wa jumuiya ya Watanzania Italia (In Campania). Zoezi hilo la kihistoria lilishuhudiwa na viongozi,wajumbe na wanajumuiya, pamoja nao pia alikuwepo Mwenyekiti wa kamati ya Diaspora nchini Italia ndugu Kagutta N.Maulidi.

Bi Judith Joseph Njozi Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Watanzania Italia, aliwashukuru wote walio hudhuria makabidhiano hayo na shukrani za kipekee alimshukuru mwenyekiti mstaafu ndugu Abdulrahaman Alli Abdallah.

Katika kukamilisha zoezi hilo, Mwenyekiti alisisitiza umoja na ushirikiano na kuwataka wanajumuiya wote kuunga mkono Uongozi ili uweze kutekeleza na kutimiza matarajio mapya ya wanajumuiya.

Pamoja na mwenyekiti pia katika makabidhiano hayo alikuwepo Katibu wa Jumuiya Bi Cecilia Lemmah na mweka hazina Bi Josephine Lello Chuwa.

Waliohudhuria wote walisaini fomu ya makabidhiano hayo ikiwa ni ishara ya ushuhuda wa kuwepo katika tukio hilo la kihistoria.

TUKIO KATIKA PICHA




















Post a Comment

0 Comments